Jumapili 18 Mei 2025 - 08:18
António Guterres akosoa vikali kuhusiana na kutojali kwa jamii ya kimataifa dhidi ya mateso yasiyo na kikomo wanayo yapitia watu wa Ghaza

Hawza/ Mkutano wa thelathini na nne wa nchi kuu za Kiarabu ulianza rasmi siku ya Jumamosi huku nchi ya Iraq wakiwa ndio wenyeji wa mkutano huo, mkutano huo ulikuwa na kaulimbiu isemayo: “Majadiliano, Ushirikiano na Maendeleo.”

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, António Guterres, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, katika matamshi yake huku akigusia migogoro inayoendelea katika eneo la Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini, alitoa wito wa kuheshimiwa kwa mamlaka ya nchi, kusitishwa kwa mapigano, na kuungwa mkono mchakato wa amani na uthabiti.

Guterres, akisisitiza ukali wa janga la kibinadamu katika Ukanda wa Ghaza, alibainisha kuwa: “Hakuna uhalali wowote wa kuwatesa na kuwafukuza watu wa Palestina. Tunaukosoa vikali muendelezo wa kuwafukuza watu wa Ghaza.”

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha